Michezo

Ibrahimovic Aanza makeke Marekani

0
Ibrahimovic Aanza makeke Marekani
Zlatan Ibrahimovic

Mshambuliaji mpya wa LA Galaxy, Zlatan Ibrahimovic, ameanza kuonyesha makeke katika Ligi Kuu ya Marekani, baada ya juzi kufunga mabao mawili na kuinyamazisha Los Angeles FC mabao 3-2.

Ibrahimovic aliondoka Manchester United hivi karibuni na kutimkia kwenye Ligi kuuu ya Marekani.

Nyota huyo aliumia mwishoni mwa msimu uliopita na kulazimika kufanyiwa upasuaji ambao ulimweka nje ya dimba kipindi kirefu.

Alianza kuonyesha makali yake katika mchezo huo wa kwanza tangu atue Marekani katika kikosi hicho.

Zlatan Ibrahimovic Marekani
Zlatan Ibrahimovic akisherekea baada ya Kufunga

Hata hivyo, Straika huyo ambaye ni raia wa Sweden, alisema anatarajia kufanya makubwa zaidi katika kikosi hucho msimu huu.

Ameshukuru kupokelewa vyema na wachezaji wenzake na kwamba lengo lake ni kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi kwenye kila mchezo.

Soma pia:  Rihanna na Jay Z waibuka tena pamoja

“Nimenza vizuri baaada ya kupata ushirikiano kutoka kwa wenzangu, nina imani nitaendeleza rekodi yangu,” alisema Straika huyo Zlatan Ibrahimovic.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo