Top Stories

Namibia kuanza kutumia Passport za Kielektroniki

0
Namibia kuanza kutumia Passport za Kielektroniki
Passport ya Namibia

Namibia imestopisha zoezi la utoaji wa passport zinazotumia mfumo wa mashine na kuanza kutoa pasipoti ambazo za kielektroniki kwanzia kesho tarehe 8 januari 2018.

Mkurugenzi wa Mambo ya Ndani, Uhamiaji na Udhibiti Mipaka, Nehemia Nghishekwa, siku ya ijumaa wiki hii katika mkutano wa wandishi wa habari huko mji Windhoek, Namibia.

Nghishekwa ameelezea kuwa passport za kielectroniki ni nyaraka salama zaidi zakusafiria na zina chip ambayo huongeza usalama.

“Lengo ni kudumisha uadilifu wa hati za kusafiria za Wanamibia na iwe vigumu mtu kufoji” Aliongea Nghishekwa.

Alisema mwenendo huo ni pamoja na kuwa sambamba na mahitaji ya International Civil Aviation Organization (ICAO). Ambayo inahimiza nchi zote za Umoja wa Mataifa kutumia passport za kielektoriniki.

Soma pia:  Rabbi wa Israel kuwakashifu Waafrika

Vipengele vya passport za kielektroniki ni pamoja na kuwepo kwa ramani ya Namibia katika cover page, picha za Bunge la Namibia, Ua la taifa la nchi ya Namibia, welwitschia mirabilis na watermark katika kurasa zote.

“Passport zilizopo sasa za mashine bado zinakubalika kimataifa” Aliongea Nghishekwa.

Passport za kielektroniki zitagharimu kiasi cha dola $160 zakinamibia ambazo sawa na (Tsh 30,000) na mda wa kusubiria kuipata pasipoti hio utakuwa ni ule ule wa awali.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories