Michezo

Michael Carrick kustaafu Msimu huu

0
Michael Carrick kustaafu Msimu huu
Michael Carrick

Michael Carrick anatarajia kustaafu mwishoni mwa msimu huu akiwa na umri wa miaka 36.

Carrick amecheza jumla ya mechi 463 akiwa na Man United tangu ajiunge na Klabu hiyo mwaka 2006 akitokea Klabu ya Tottenham kwa kitita cha Paundi milioni 18 ambayo sawa na Billioni 56 za kitanzania.

“Kuna wakati ukifika, mwili wako unakuambia kuwa sasa ni mda wa kupumzika. Na sasa niko katika mda huo”. Alisema Carrick

Carrick aliweza kuibuka na Mataji yafuatayo:-

1Ligi kuu ya Uingereza5
2Ligi ya mabingwa Ulaya1
3Kombe la Europa 1
4Kombe la FA 1
5Kombe la Ligi ( EFL )3
6Klabu Bingwa ya Dunia1

Meneja Jose Morinho alisema Januari kuwa Carrick atachukuwa ofa ya ukocha mwishoni mwa msimu

Michael Carrick kustaafu Msimu huu
Michael Carrick
Soma pia:  Real Madrid wakomaa na Pogba

Comments

Comments are closed.

More in Michezo